• HABARI MPYA

    Friday, December 17, 2021

    SIMBA YAZINDUA MICHANGO UJENZI WA UWANJA WAKE


    KLABU ya Simba leo imezindua rasmi kampeni za ujenzi wa Uwanja wake kwa ajili ya mechi za mashindano ya ndani na kimataifa.
    Kampeni hiyo imezinduliwa jioni ya leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.
    Waliozindua kampeni hiyo ni Mwenyekiti wa Wanachama wa klabu hiyo, Murtaza Ally Manungu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.


    Mpango huu ni wazo la Mwanahisa mkuu Simba, Mohamed 'Mo' Dewji ambaye ameahidi kutoa Sh. Bilioni 2 ili wanachama wajazie klabu hiyo ijenge Uwanja wake kuepuka adha inazokutana nao kutumia Uwanja usio wake.
    Kwa sasa Simba ina Uwanja wa mazoezi tu, Mo Simba Arena uliopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na mechi zake za mashindano inatumia Uwanja wa Benjamin Mkapa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA YAZINDUA MICHANGO UJENZI WA UWANJA WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top