• HABARI MPYA

  Monday, December 20, 2021

  CHIPUKIZI MWINGINE MTANZANIA ASAJILIWA LIGI YA ISRAEL


  MSHAMBULIAJI CHIPUKIZI Mtanzania, Omary Ally Marungu amesajiliwa na klabu ya 
  Hapoel Kfar Saba FC ya Israel kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.
  Mchezaji huyo aliyeng'ara katika ligi ya vijana ya U20 msimu uliopita akiiwezesha Mtibwa Sugar kutwaa ubingwa amesajiliwa na klabu hiyo ya Daraja la Kwanza Israel, ijulikanayo kama
  Liga Leumit baada ya kufuzu majaribio aliyofanya kuanzia mapema mwezi huu.
  Anakuwa Mtanzania mwingine kucheza Israel kwa sasa baada ya kiungo Novatus Dismas Miroshi, anayecheza teams: Beitar Tel Aviv Bat Yam FC ya Liga Leumit pia kwa mkopo kutoka 2021 Maccabi Tel Aviv aliyojiunga nayo mwaka jana kutoka Azam FC ya Dar es Salaam.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHIPUKIZI MWINGINE MTANZANIA ASAJILIWA LIGI YA ISRAEL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top