• HABARI MPYA

    Saturday, December 18, 2021

    SIMBA YAIKATAA RASMI GSM LIGI KUU


    SIMBA ndio klabu pekee kati ya 16 iliyopinga udhamini wa kampuni ya GSM katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
    Katika mkutano uliofanyika jana baina ya Uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na klabu ya 16 za Ligi Kuu, mambo mbali mbali yalijadiliwa ikiwemo udhamini wa GSM.
    Novemba 23, mwaka huu GSM iliingia mkataba wa Udhamini Mwenza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa dau la Sh. Bilioni 2.1 kwa miaka miwili.


    Mapema baada ya TPLB kutangaza udhamini wa GSM katika Ligi Kuu, Simba iliiandikia barua ya kuhoji juu ya mkataba wa udhamini wa kampuni hiyo, huku pia wakiwa wadhamini wa wapinzani wao, Yanga SC.
    Katika barua hiyo iliyosainiwa na Mtendaji Mkuu wa Simba, klabu hiyo, Barbara Gonzalez ilisema haifahamu kwa undani juu ya mkataba huo wao watanufaika vipi zaidi tu ya kufahamishwa kutumia nembo ya GSM kwenye tiketi na jezi zao wakati wa mechi za ligi hiyo.
    Lakini pia Simba ilisema GSM kuwa wadhamini wa Ligi Kuu wazi inaleta mgongano wa kimslahi kwa sababu ni wadhamini wa Yanga pia, klabu ambayo kwa pamoja na mdhamini wao lengo lao ni kutwaa ubingwa wa ligi kama wao. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA YAIKATAA RASMI GSM LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top