• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 07, 2021

  SIMBA SC WAREJEA DAR KUWAVAA WATANI JUMAMOSI


  KIKOSI cha Simba SC kimerejea Dar es Salaam kwa maandizi ya mwisho kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.


  Simba ilikuwa Zambia tangu Ijumaa ambako walikwenda kumenyana na wenyeji, Red Arrows katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, ambao walifungwa 2-1 Jumapilu, lakini wamefuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 4-2 kufuatia kushinda 3-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam.

  Wakati wakisubiri kurejea Dar es Salaam leo, Simba jana ilifanya mazoezi Lusaka ili kuwaweka fiti wachezaji wake.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAREJEA DAR KUWAVAA WATANI JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top