• HABARI MPYA

  Tuesday, December 21, 2021

  WAZIRI AWAPONGEZA TANZANITE KUSONGA MBELE KOMBE LA DUNIA


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amekutana na wachezaji wa timu ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite kwa kufuzu Raundi ya Tatu ya kufuzu Kombe la Dunia mwakani.
  Tanzanite imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3 baada ya kushinda 3-2 katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam kabla ya sare ya 1-1 Bujumbura Jumapili na sasa itamenyana na Ethiopia katika Raundi ya Tatu.  Kabla ya mechi ya marudiano wachezaji 11 wa Tanzanite waliambiwa wana maambukizi ya virusi vya Corona, hivyo kulazimika kucheza nane muda wote.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI AWAPONGEZA TANZANITE KUSONGA MBELE KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top