• HABARI MPYA

    Friday, December 10, 2021

    CAF YAZUIA MABANGO YA GSM SIMBA NA YANGA KESHO


    SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeliagiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoweka mabango ya wadhamini wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, GSM katika mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Hatua hiyo inafuatia malalamiko waliyopokea kutoka kwa Simba SC juu ya udhamini wa GSM, ambao pia ni wadhamini wa wapinzani wao, Yanga.


    Awali, Simba iliiandikia barua Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) kuhoji juu ya mkataba wa udhamini wa kampuni ya GSM katika Ligi Kuu huku pia wakiwa wadhamini wa wapinzani wao, Yanga SC.
    Katika barua hiyo iliyosainiwa na Mtendaji Mkuu wa Simba, klabu hiyo imesema haifahamu kwa undani juu ya mkataba huo wao watanufaika vipi zaidi tu ya kufahamishwa kutumia nembo ya GSM kwenye tiketi na jezi zao wakati wa mechi za ligi hiyo.
    Lakini pia Simba ilisema GSM kuwa wadhamini wa Ligi Kuu wazi inaleta mgongano wa kimslahi kwa sababu ni wadhamini wa Yanga pia, klabu ambayo kwa pamoja na mdhamini wao lengo lao ni kutwaa ubingiwa ligi kama wao.
    Novemba 23, mwaka huu GSM iliingia mkataba wa Udhamini Mwenza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa dau la Sh. Bilioni 2.1 kwa miaka miwili.
    Na barua ya CAF leo imeagiza matumizi yote ya nembo za mdhamini huyo mpya yasitishwe hadi hapo itakapoifanyia kazi kesi hiyo na kutoa uamuzi.
    Mapema leo, kocha wa Simba, Mspaniola Pablo Franco Martin aligoma kushiriki mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wa kesho kwa sababu ya kuwepo mabango ya GSM nyuma ya meza.
    Na baada ya barua ya CAF, mabango yote ya GSM yaliyokuwa yamekwishawekwa Uwanja wa Mkapa yameondolewa.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAF YAZUIA MABANGO YA GSM SIMBA NA YANGA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top