• HABARI MPYA

  Tuesday, December 21, 2021

  MTIBWA YALAZIMISHWA SARE NA POLISI 1-1 GAIRO


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wamelazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Shabiby huko mjini Morogoro.
  Vitalis Mayanga alianza kuifungia Polisi dakika ya 14, kabla ya Datius Peter kujifunga dakika ya 57 kuipatia Mtibwa bao la kusawazisha. 
  Kwa sare hiyo, Mtibwa inafikisha pointi saba na inaendelea kushika mkia, wakati Polisi imetimiza pointi 16 na kurejea nafasi ya tatu baada ya timu zote kucheza mechi 10 sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA YALAZIMISHWA SARE NA POLISI 1-1 GAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top