• HABARI MPYA

  Monday, December 27, 2021

  SIMBA QUEENS YASHINDA 8-0, YANGA PRINCESS YADROO


  MABINGWA watetezi, Simba Queens wameendelea kugawa maumivu kwa wapinzani katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya kuichapa Oysterbay Girls 8-0 jioni ya leo Uwanja wa Mo SIMBA Arena, Bunju, Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Aisha Djafar matatu, Opa Clement na Aisha Mnunka kila mmoja mawili, wakati la nane Oysterbay Girls walijifunga.
  Watani wao, Yanga Princess wamelazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Fountain Gate Princess Uwanja wa Fountain Gate, Dar es Salaam.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS YASHINDA 8-0, YANGA PRINCESS YADROO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top