• HABARI MPYA

  Thursday, December 23, 2021

  YANGA KUNDI B, SIMBA KUNDI C MAPINDUZI CUP 2022


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wamepangwa Kundi B katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2022 pamoja na wenyeji, Taifa Jang’ombe na KMKM zote za Zanzibar.
  Washindi wa pili wa msimu uliopita, Simba SC wao wapo Kundi C pamoja na wenyeji watupu pia, Sellem View na Mlandege FC, wakati Kundi A lina timu mbili za kila upande, Azam FC na Namungo za Bara na Yosso Boys na Meli City za Zanzibar.
  Michuano hiyo itaanza Jumapili ya Januari 2, mwakani na Simba watacheza Januari 6 dhidi ya Sellem View, wakati Yanga watamenyana na Taifa siku inayofuata mechi zote zikipigwa Uwanja wa Amaan.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KUNDI B, SIMBA KUNDI C MAPINDUZI CUP 2022 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top