• HABARI MPYA

  Friday, December 17, 2021

  MKULIMA ASHINDA JACKPOT BONUS YA MILIONI 10

  MKAZI wa Ifakara, Kilombero Mkoani Morogoro, Bwana Kassim Said Linzio, amekuwa ni mmoja wa washindi wa bonasi ya Jackpot ya Sportpesa wawiki hii kwa kuibuka na kitita cha shilingi Milioni Kumi (10).
  Bwana Kassim, ambaye ana umri wa miaka 51, ni mmoja kati ya washindi saba, kati ya walioshinda bonus ya Sportpesa Jackpot wiki hii, kwa kubashiri kwa usahihi timu 12 kati ya 13.
  Bwana Kassim anasema alianza kucheza na Sportpesa Mwezi Juni 2020, baada ya kusikia kutoka kwa jamaa zake wa karibu na kuona matangazo kupitia simu yake ya kitochi.
  Mimi nilianza kucheza mdogo mdogo, kwa kubashiri timu tano mpaka saba, na kushinda mara kwa mara, kati ya shilingi elfu arobaini na elfu sabini. Baada ya hapo nilipata tamaa ya kujaribu na kucheza mechi nyingi Zaidi”.


  Anaendelea kwa kusema baada ya kuona uwezo wake wa kubashiri na kupatia mechi nyingi umefikia wastani wa mechi 11 hadi 12, aliona ni afadhali ajaribu Jackpot, kwa kuwa ina kiwango cha juu cha malipo.
  Baba huyu mwenye familia yenye mke mmoja, na watoto watano, anajishughulisha zaidi na shughuli ya kilimo cha mpunga na upasuaji wa kokoto alipata meseji ya ushindi siku ya Tarehe 13, jioni.
  ‘’Nakumbuka nilipopata meseji ya ushindi, nilipiga simu SportPesa, kwa kutumia namba ya huduma kwa wateja, na kuhakikishiwa kuwa ni kweli nimeshinda na hivyo nitahitajika kwenda kwenye ofisi za SportPesa kwa ajili ya utaratibu wa malipo’’.
  Ingawa ndoto ya bwana Kassim ilikuwa kushinda Jackpot kubwa ambayo kwa sasa ni zaidi ya shillingi 783,781,040 ushindi huu umempa ari zaidi ya kucheza na kuifukuzia Jackpot hiyo.
  ‘’Ni malengo yangu kwamba niliitaka ile jackpot kubwa, lakini kwa kuwa nimepata bonus, basi nitafanya yale machache yaliyokuwa kiporo katika malengo yangu ya muda mfupi, wakati huo huo nikijitahidi kupambana kwa ajili ya Jackpot kubwa’’.
  Akimalizia bwana Kassim anasema pesa aliyoipata itamsaidia kumalizia nyumba yake, Kulipa ada za shule za watoto wake na pia kumpatia mkewe mtaji kwa ajili ya biashara atakayoona inamfaa.
  Pia amewaasa watanzania hasa hasa watu wenye umri kama wake kuona kucheza michezo hii ya kubashiri kama fursa ya kuongeza kipato na kujaribu bahati yao. “Nitoe rai kwa wananchi wenzangu na watanzania wote kwa ujumla wacheze na Sportpesa kwani huduma zao ni nzuri na malipo ni ya uhakika’’.
  Kutoka SportPesa Meneja Uhusiano na Mawasiliano Sabrina Msuya aliongeza kwa kusema “Tunampongeza sana Kassim Pamoja na washindi wa wiki hii wote kwa kupata Jackpot bonus.”
  “Hii ni ishara nzuri na kwamba nafasi ya ushindi ni kubwa na hivi karibuni bila shaka tutampata mshindi”
  “Sportpesa inawakaribisha wateja wapya na endelevu kuendelea kucheza Jackpot kubwa na kujipatia ushindi”.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKULIMA ASHINDA JACKPOT BONUS YA MILIONI 10 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top