• HABARI MPYA

  Thursday, December 23, 2021

  SIMBA QUEENS YASHINDA 15-0 LIGI YA WANAWAKE


  MABINGWA watetezi, Simba Queens wameanza vyema Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya ushindi wa 15-0 dhidi ya Ruvuma Queens jioni ya leo Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju   Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Zena Khamis matatu, Asha Djafar matatu, Opa Clement matatu, Jacqueline Albert matatu, Aisha Juma na mawili Ruvuma Queens walijifunga.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara leo, wenyeji, Alliance Girls wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mlandizi Queens Uwanja Nyamagana Jijini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS YASHINDA 15-0 LIGI YA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top