• HABARI MPYA

  Saturday, December 18, 2021

  AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA MBEYA CITY CHAMAZI


  WENYEJI, Azam FC wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yote l yamefungwa na Wazimbabwe, beki Bruce Kangwa dakika ya 13 na kiungo Never Tigere dakika ya 73, wakati ya Mbeya City yamefungwa na washambuliaji Juma Luizio dakika ya 28 Richardson Ng'odya dakika ya 65.
  Azam FC inafikisha pointi 12 katika nafasi ya saba na Mbeya City sasa ina pointi 15 na kupanda nafasi ya tatu baada ya timu zote kucheza mechi tisa sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA MBEYA CITY CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top