• HABARI MPYA

  Monday, December 27, 2021

  MBEYA CITY, KWANZA ZATOA SARE UGENINI LIGI KUU


  WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya 1-1 na Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
  Geita walitangulia kwa bao la penalti la George Mpole dakika ya 51, kabla ya Habib Kyombo kuisawazishia Mbeya Kwanza dakika ya 81.
  Kwa sare hiyo katika mechi ya 11, Geita Gold inafikisha pointi 12, ingawa inabaki nafasi ya tisa, ikizidiwa wastani wa mabao na Namungo FC yenye mechi moja mkononi pia.
  Kwa upande wao, Mbeya Kwanza wanafikisha pointi 11 na kusogea nafasi ya 10, wakiizidi wastani wa mabao tu Tanzania Prisons inayohamia nafasi ya 11.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Polisi Tanzania imelazimishwa sare 0-0 na Mbeya City Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
  Kwa sare hiyo kwenye mechi ya 11 kwa timu zote, Polisi Tanzania inafikisha pointi 17, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Mbeya City inatimiza pointi 16 na kurejea nafasi ya nne ikiizidi wastani wa mabao tu Dodoma Jiji FC ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY, KWANZA ZATOA SARE UGENINI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top