• HABARI MPYA

  Tuesday, December 28, 2021

  MAFUNDI WANAPOKUTANA, HESHIMA HUCHUKUA NAFASI YAKE


  VIUNGO, Mganda Khalid Aucho (28) wa Yanga na Ramadhan Chombo ‘ Redondo’ wa Biashara United (34) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-1.
  Wawili hawa waliibuka pamoja mwaka 2009, Redondo akitokea Ashanti na akacheza pia Simba, Azam FC, Villa Squad, Mbeya City, Friends Rangers na African Lyon kabla ya kujiunga na Biashara mwaka 2019.
  Kwa upande wake Aucho aliibukia Manispaa ya Jinja, akacheza hadi Maji (Water), Simba za kwao, Uganda, Tusker, Gor Mahia za Kenya, Baroka FC ya Afrika Kusini, Red Star Belgrade, OFK Beograd za Serbia, East Bengal, Churchill Brothers za India na El Makkasa ya Misri kabla ya kutua Yanga Agosti mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAFUNDI WANAPOKUTANA, HESHIMA HUCHUKUA NAFASI YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top