• HABARI MPYA

  Friday, December 24, 2021

  YANGA PRINCESS WASHINDA 2-0 DOM LIGI YA WANAWAKE


  TIMU ya Yanga Princes imeanza vyema Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Bao Bab Queens Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Mabao yote ya Yanga Princes leo yamefungwa na mshambuliaji chipukizi wa kimafaifa wa Tanzania, Aisha Masaka yote kipindi cha pili.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu ya Wanawake leo, JKT Queens imeichapa Oysterbay Girls 3-1 Uwanja wa Meja Jenerali Isamhuyo, Mbweni, The Tigers Queens wameichapa TSC Queens 4-0 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na Fountain Gate Princess wameshinda 4-0 dhidi ya Ilala Queens Uwanja wa Fountain Gate, Dar es Salaam.
  Ikumbukwe jana mabingwa watetezi, Simba Queens, 
  walishindi wa 15-0 dhidi ya Ruvuma Queens Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju   Jijini Dar es Salaam, mabao yake yakifungwa na Zena Khamis matatu, Asha Djafar matatu, Opa Clement matatu, Jacqueline Albert matatu, Aisha Juma na mawili Ruvuma Queens walijifunga.
  Mechi nyingine ya jana, wenyeji, Alliance Girls walishindi wa 1-0 dhidi ya Mlandizi Queens Uwanja Nyamagana Jijini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA PRINCESS WASHINDA 2-0 DOM LIGI YA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top