• HABARI MPYA

  Tuesday, December 28, 2021

  MSUVA APANGWA NA ZAMALEK NA TIMU MBILI ZA ANGOLA

  NYOTA wa Tanzania, Simon Happygod Msuva, timu yake, Wydad Athletic ya Morocco, maarufu Wydad Casablanca imepangwa Kundi D katika Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Zamalek ya Misri, Petro Atletico na GD Sagrada Esperanca za Angola.
  Mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri wamepangwa Kundi A pamoja na timu ya zamani ya kocha wao, Pitso Mosimane
  Mamelodi Sundowns ya nyumbani kwao, Afrika Kusini na Al Hilal na Al Merriekh, zote za Sudan.
  Kundi B linaundwa na Raja Athletic ya Morocco pia, Horoya ya Guinea, ES Setif ya Algeria na AmaZulu ya Afrika Kusini, wakati Kundi C kuna
  Esperance na Etoile du Sahel, zote za Tunisia, CR Belouizdad ya Algeria na Jwaneng Galaxy ya Botswana.
  Msuva mwenye umri wa miaka 26 sasa, aliibukia Azam Academy mwaka 2010, kabla ya kucheza Moro United 2011 hadi 2012 alipohamia Yanga ambayo aliichezea hadi mwaka 2017 aliponunuliwa na Difaâ El Jadida ya Morocco pia alikocheza hadi 2020 aliponunuliwa na Wydad.
  Hadi sasa, Msuva ameichezea timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ mechi 73 na kuifungia mabao 17.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA APANGWA NA ZAMALEK NA TIMU MBILI ZA ANGOLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top