• HABARI MPYA

  Wednesday, December 22, 2021

  DODOMA JIJI WAILAZA NAMUNGO FC 2-1 ILULU


  WENYEJI, Namungo FC wamekubali kipigo cha 2-1 kutoka kwa Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
  Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na Anuary Jabir dakika ya 18 na Emmanuel Martin dakika ya 73, wakati la Namungo FC limefungwa na Bigirimana Blaise dakika ya 26.
  Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 16 katika nafasi ya nne, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 12 katika nafasi ya saba baada ya timu zote kucheza mechi 10.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, wenyeji wengine, Kagera Sugar wamechapwa mabao 2-0 na Mbeya Kwanza Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Mabao ya Mbeya Kwanza jioni ya leo yamefungwa na Willy Edgar dakika ya 36 na Oscar Mwajanga dakika ya 85 na kwa ushindi huo inafikisha pointi 10 katika mechi ya 10 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Kagera inabaki na pointi zake tisa za mechi tisa nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI WAILAZA NAMUNGO FC 2-1 ILULU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top