• HABARI MPYA

  Sunday, December 05, 2021

  KMC NA COASTAL ZASHINDA NYUMBANI LIGI KUU


  TIMU ya KMC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya KMC leo yamefungwa na Abdulrazak Hamza dakika ya 47 na Matheo Anthony dakika ya 59.
  Kwa ushindi huo, KMC imefikisha pointi tisa na kusogea nafasi ya nane, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake tano katika nafasi ya 25 kwenye Ligi ya timu 26, baada ya wote kucheza mechi nane.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, wenyeji, Coastal Union wameichapa timu nyingine iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, Mbeya Kwanza mabao 2-1 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanya.
  Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Vincent Abubakar dakika ya pili na Amani Kyata dakika ya 76, wakati la Mbeya Kwanza limefungwa na Willy Edgar dakika ya 48.
  Coastal Union inatimiza pointi 11 na kupanda nafasi ya sita, wakati Mbeya Kwan inabaki na pointi zake  saba katika nafasi ya 13 baada y timu zote kucheza mechi nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC NA COASTAL ZASHINDA NYUMBANI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top