• HABARI MPYA

  Sunday, December 05, 2021

  SIMBA SC YATINGA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO


  MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamefanikiwa kufuzu Hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya kuchapwa mabao 2-1 na wenyeji, Red Arrows jioni ya leo Uwanja wa Taifa wa Mashujaa Jijini Lusaka, Zambia.
  Mabao ya Red Arrows yamefungwa na Ricky Banda dakika ya 45 na Sadam Phiri dakika ya 48, wakati bao pekee la Simba SC limefungwa na Hassan DIlunga dakika ya 67.
  Simba SC inaingia hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 4-2 kufuatia kushinda 3-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATINGA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top