• HABARI MPYA

  Saturday, October 02, 2021

  TWIGA STARS YATINGA NUSU FAINALI COSAFA


  TIMU ya taifa ya wanawake, Twiga Stars imeingia Nusu Fainali ya Kombe la COSAFA baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana kwenye mchezo wa Kundi B leo Uwanja wa  Nelson Mandela Bay Jijini Port Elizabeth, Afrika Kusini.
  Mabao ya Tanzania leo yamefungwa na Deonisia Minja dakika ya sita na Mwanahamisi Omary dakika ya 79 na kwa matokeo hayo Twiga Stars inafikisha pointi sita kufuatia kuichapa na Zimbabwe 3-0 kwenye mechi ya kwanza Jumatano.


  Beki Famta Issa ‘Densa’ amechaguliwa Mchezaji wa Bora wa mechi hiyo kama ilivyokuwa kwenye mechi ya kwanza Mwanahamisi Omary alishinda tuzo hiyo dhidi ya Zimbabwe.
  Twiga Stars inayofundishwa na kocha Bakari Shime itakamilisha mechi zake za Kundi B kwa kumenyana na Sudan Kusini Jumatatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS YATINGA NUSU FAINALI COSAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top