• HABARI MPYA

  Saturday, October 02, 2021

  AZAM FC YACHAPWA 2-1 MOSHI


  WENYEJI, Polisi Tanzania wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Mabao ya Polisi leo yamefungwa na Kassim Shaaban dakika ya 23 na Adam Adam dakika ya 40, wakati la Azam FC limefungwa na Iddi Suleiman 'Nado'.
  Ni ushindi wa pili kwa Maafande wa Jeshi la Usalama wa Raia baada ya kuichapa KMC 2-0 kwenye mechi ya kwanza Karatu, wakati Azam FC wanafikisha mechi mbili bila ushindi, kufuatia kutoa sare ya 1-1 na Coastal Union Jijini Tanga.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Coastal Union imetoa sare ya pili mfululizo nyumbani, 0-0 na KMC Uwanja wa Mkwawani, Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YACHAPWA 2-1 MOSHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top