• HABARI MPYA

  Friday, September 03, 2021

  SIMBA QUEENS YASHINDA 10-0 CECAFA SAMIA CUP

   TIMU ya Simba Queens imefanikiwa kwenda Nusu Fainali baada ya ushindi wa 10-0 dhidi ya FAD FC ya Djibouti katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi A Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ya Wanawake, CECAFA Samia Cup leo Uwanja wa Moi Kasarani Jijini Nairobi, Kenya.
  Mabao ya Simba Queens leo yamefungwa na winga Mkongo, Flavian Mawete Musolo dakika ya tano, 38 na 46, Opa Clement Sanga dakika ya 20, 44 na 50, Aisha Juma Mnunka dakika ya 28 na 35, Asha Jaffar dakika ya 31 na 86.
  Simba Queens inamaliza mechi za Kundi lake na pointi saba baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya PVC ya Burundi na sare ya 0-0 na Lady Doves WFC ya Uganda.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS YASHINDA 10-0 CECAFA SAMIA CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top