• HABARI MPYA

  Tuesday, September 07, 2021

  MTIBWA SUGAR YAENDELEA KUSAJILI CHIPUKIZI LIGI KUU

   MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Mtibwa Sugar wameendeleza sera yao ya kusajili wachezaji vijana wadogo kuelekea msimu ujao.


  Mtibwa, mabingwa mara mbili mfululizo 1999 na 2000 wamemsajili winga wa kushoto Isaac Kachwele kutoka akademi ya Cambianso ya Temeke Jijini Dar es Salaam.


  Wakati Miwa hao wa Manungu pia wamemsajili kiungo George Chotta aliyeibukia akademi ya Moro Kids na kucheza Kitayosce na Mbeya City.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAENDELEA KUSAJILI CHIPUKIZI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top