• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 24, 2018

  MBEYA CITY WAENDA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI MALAWI KESHO

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  KIKOSI cha Mbeya City kesho kinatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Karonga United iliyopanda ligi kuu ya Malawi.
  Timu hiyo ya Mbeya inaondoka kesho asubuhi kuelekea Malawi kwa ajili ya mchezo huo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Azam FC unatarajiwa kupigwa Aprili 8 mwaka huu uwanja wa Sokoni, Mbeya.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo, kocha mkuu wa timu hiyo, Mrundi Ramadhani Nsanzurimo alisema mechi hiyo ni kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao na Azam ili kupata pointi muhimu.
  Alisema mbali na kuwepo mechi hiyo pia atakuwa na mechi mbili za kirafiki ikiwemo Majimaji au njombe Mji pamoja timu ya Mbinga United.
  "Nimefanya mazoezi kwa muda mrefu sasa ni muda wa kuona nilichokifanya wanakifanyia kazi, sehemu ya kuona kupitia mechi hizi za kirafiki," alisema.
  Nsanzurimo alisema maandalizi ya mechi hiyo ni kujiandaa michezo minne mfululizo baada ya Azam, wanatarajia kucheza na Yanga.
  "Hizi mechi za kirafiki zitatusaidia ukizingatia, tunahitaji pointi muhimu katika michezo yetu tutakayocheza nyumbani,"alisema kocha huyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBEYA CITY WAENDA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI MALAWI KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top