• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 31, 2018

  KUMEKUCHA TUZO ZA FILAMU TANZANIA, RAIS MSTAAFU JK MGENI RASMI KESHO MLIMANI CITY

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  RAIS mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tuzo ya filamu bora itayofanyika kesho usiku, katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
  Katika tuzo hizi kutakuwa watu maarufu kutoka Serikalini pamoja na wasanii  ndani na nje ya nchi huku msanii wa kihindi wa kike Preetika Rao maarufu kama 'Aaliyah', atakuwa miongoni mwa wageni maalum.
  Aaliyah aliwasili nchini jana na tayari kwa ajili ya shughuli hiyo akiambatana na wasanii maarufu akiwemo Nassib Abdul 'Diamond', Hamisa Mobeto na wengine kutoka Kenya, Zambia, Uganda na Rwanda.
  Preetika Rao au 'Aaliyah' (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari leo ofisi za Azam TV, Tabata mjini Dar es Salaam

  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online, Mkuu wa Channel za Azam, Fatuma Mohammed alisema mbali na wageni hao watakaokuwepo katika tuzo hiyo  pia atakuwepo Waziri wa Habari utamaduni sanaa na michezo, D. Harrison Mwakyembe.
  Alisema tuzo hiyo za kwanza kubwa hapa nchini kufanyiwa,  iliyojikita katika kuibua na kuendeleza tasnia ya sanaa ya maigizo na filamu shiriki kutoka Tanzania, Kenya, Rwanda, Burundi na DRC.
  “ Filamu hizo kutoka nchini , zinazowania na kuondoka na Tuzo, pesa taslimu, kutakuwa utambulisho maalum na wakipekee kwenye soko la filamu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na Nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara " alisema Fatuma.
  Alisema katika tuzo hiyo kutakuwa na filamu bora, mwandishi bora wa filamu na  msainii bora wa kike na kiume.
  “Tuzo hizo ni tofauti kabisa na zingine kwani mbali na mshindi kuchukuwa tuzo pia washindi watapewa fedha, thamani ya zawadi ni million 4," alisema. 
  Fatuma alisema mbali na Tuzo hizo lakini pia Aliyah atazindua Channel ya Sinema zetu ambayo kwa sasa imeboreshwa na kuwa na muonekano mpya. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KUMEKUCHA TUZO ZA FILAMU TANZANIA, RAIS MSTAAFU JK MGENI RASMI KESHO MLIMANI CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top