• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 30, 2018

  EMMANUEL OKWI AREJEA LEO KUKAMILISHA KIKOSI CHA SIMBA SAFARI YA NJOMBE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
  MSHAMBULIAJI tegemeo wa Simba SC, Emmanuel Okwi anatarajiwa kutua leo nchini na kujiunga na kikosi cha timu hiyo kinachoondoka kesho mjini Dar es Salaam kwenda Iringa tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Njombe Mji.
  Timu hizo zinatarajia kukutana Aprili 3, Mwaka huu mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Saba Saba mjini humo na akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Meneja wa Simba, Richard Robert amesema kwamba mara atapowasili, Okwi ataungana na wachezaji wenzake kwa safari ya Iringa mapema kesho.
  Emmanuel Okwi anatua leo kujiunga na kikosi cha Simba SC kwa safari ya Iringa kesho

  Kikosi cha Simba SC chini ya kocha wake Mkuu, Mfaransa Pierre Lechantre kinaondoka mapema kesho kwenda Iringa kuweka kambi siku mbili kujiandaa na mchezo dhidi ya Njombe Mji FC.
  Okwi pamoja na Mganda mwenzake, beki Juuko Murshid walikuwa kwenye timu yao ya taifa, ambayo ilikuwa na mechi mbili za kirafiki katikati ya wiki, ikishinda 3-1 dhidi ya Sao Tome e Príncipe Machi 24 na sare 0-0 na Machi 27 Uwanja wa Mandela mjini Kampala.
  Lakini Juuko yuko nchini tangu juzi, ingawa haijulikani kilichomfanya Okwi akachelewa.
  Meneja huyo alisema wachezaji watakaokuwepo katika msafara huo pamoja na Salim Mbonde na Haruna Niyonzima ambao walikuwepo majeruhi na sasa kurejerea kikosini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: EMMANUEL OKWI AREJEA LEO KUKAMILISHA KIKOSI CHA SIMBA SAFARI YA NJOMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top