• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 30, 2018

  MTIBWA SUGAR KUWAKOSA BABA UBAYA NA KANONI MECHI NA AZAM KESHO CHAMAZI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mtibwa Sugar ya Morogoro itawakosa wachezaji wake wawili, wote mabeki wa pembeni, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ na Salum Kanoni katika mchezo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federationa Cup (ASFC) dhidi ya Azam FC kesho.
  Mtibwa Sugar watakuwa wageni wa Azam FC kuaniza Saa 2:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam katika Robo Fainali ya ASFC.
  Na kuelekea mchezo huo, Kocha wa timu hiyo Kocha Mkuu wa Mtibwa, Zuberi Katwila amesema kwamba wachezaji wake wengine wote wapo fiti ukiondoa mabeki wa zamani wa Simba, Baba Ubaya na Kanoni ambao watakosekana kesho.  
  Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ atakosekana katika mchezo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federationa Cup dhidi ya Azam FC kesho

  Akizungumzia mchezo huo, Katwila mchezaji wa zamani w Mtibwa, amesema; “Kila timu iliyofika hapa katika robo fainali ya kombe hili ni nzuri, hivyo tunajua tunaenda kupambana na timu  nzuri hivyo tunaenda tukijua tunapambana na timu nzuri ila tumejipanga kwa ajili ya kuwaletea furaha na heshima wana Mtibwa Sugar”.
  Robo Fainali za Azam Sports Federation Cup zinaanza jioni ya leo, Stand United wakiikaribisha Njombe Mji FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
  Kabla ya Azam FC kuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar kuanzia Saa 2:00 usiku kesho, Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa JKT Tanzania Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Aprili 1, Uwanja wa Namfua mjini Singida, Yanga watakuwa wageni wa Singida United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR KUWAKOSA BABA UBAYA NA KANONI MECHI NA AZAM KESHO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top