• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 19, 2018

  HERI MZOZO 'ALIVYOMKAZIA' HUYU MTOTO JANA HADI HURUMA!

  Mkurugenzi wa klabu ya Friends Rangers ya Daraja la Kwanza, Heri Mzozo akifuatilia mchezo wa kirafiki wa kimataifa baina ya timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Tanzania, Ngorongoro Heroes na Morocco jana Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam kiasi cha kushindwa kumskiliza mtoto aliyembeba 
  Pamoja na mtoto kumuambia hadi kwa ishara ya kidole, lakini Heri Mzozo alikuwa ameelekeza fikra zake zote kwenye mchezo ambao Ngorongoro walishinda 1-0 
  Hakika kijana huyu alipata wakati mgumu mno, kwa sababu baba hakumskiliza kabisa 
  Ikafika wakati hadi mtoto akawa kama anataka kuteremka aende kuchukua mwenyewe anachomuonyesha baba yake 
  Lakini hakuweza kuteremka kutokana na namna baba yake alivyokuwa amemshika vizuri 
  Alipozidi kutaka kujinasua, baba akamuangalia kwa jicho la ukali na mtoto akawa mpole
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HERI MZOZO 'ALIVYOMKAZIA' HUYU MTOTO JANA HADI HURUMA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top