• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 31, 2018

  MAKAMU MWENYEKITI AZAM FC APEWA UJUMBE BODI YA OLIMPIKI TANZANIA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MAKAMU Mwenyekiti wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Olimpiki Maalum Tanzania.
  Kwa mujinu wa barua ya uteuzi wake kutoka kwa Mwenyekiti wa Olimpiki Maalum Tanzania, Dk. Mwanandi Mwankemwa, Popat anakuwa Mjumbe kuanzia Machi mwaka huu.
  Na hakuna kingine kilichowasukuma Olimpiki Maalum Tanzania kumpa wadhifa huo Popat zaidi ya uadilifu wake na uwajibikaji mzuri katika majukumu yake.
  “Katika jitihada za Olimpiki Maalum Tanzania kuiimarisha Bodi yake, inachukua watu ambao inaona watatusaidia majukumu mbalimbali. Olimpiki Maalum inakuomba kuwa Mjumbe wa Bodi yake,”imesema barua hiyo.
  Abdulkarim Amin ‘Popat’ (kushoto) akiwa na Rais wa heshima wa Azam FC, Jamal Bakhresa 

  Katika mwaka wake wa kwanza tu wa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Azam FC, Popat ambaye ni mchezaji wa zamani wa klabu hiyo amewavutia wengi kwa utendaji na desturi yake nzuri.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAKAMU MWENYEKITI AZAM FC APEWA UJUMBE BODI YA OLIMPIKI TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top