• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 21, 2018

  MSUVA APEWA MAZEMBE, MC ALGER NA SETIF LIGI YA MABINGWA

  TIMU ya Difaa Hassan El Jadidi ya Moroccco imepangwa Kundi B katika Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na MC Alger na ES Setif za Algeria na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Difaa Hassan El Jadidi inayojivunia kiungo mshambuliaji Mtanzania, Simon Msuva itakwenda DRC kwa mara ya pili, kwani ili kufika hatua hii ililazimika kuitoa AS Vita ya Kinshasa.
  Kundi A linaundwa na timu za Al-Ahly ya Misri, Township Rollers ya Botswana, KCCA ya Uganda na Esperance ya Tunisia, wakati Kundi C lina timu za AS Togo-Port ya Togo, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, mabingwa watetezi Wydad Casablanca ya Morocco na Horoya ya Guinea.
  Simon Msuva (kushoto) amepangwa kundi moja MC Alger na ES Setif za Algeria na TP Mazembe ya DRC

  Kundi D linaundwa na timu za ZESCO United ya Zambia, Premiero de Agosto ya Angola, Etoile du Sahel ya Tunisia na Mbabane Swallows ya Swaziland. Mechi zinatarajiwa kuanza mwezi Mei hadi Agosti mwaka huu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSUVA APEWA MAZEMBE, MC ALGER NA SETIF LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top