• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 21, 2018

  SINGIDA UNITED WAMALIZANA NA FANJA KUHUSU DANNY LYANGA LAKINI KUCHEZA MSIMU UJAO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Singida United imesema kwamba haiwezi kumtumia mshambuliaji wake mpya, Danny Lyanga kwa sababu alichelewa kupatiwa Hati yaUhamisho wa Kimataifa (ITC kutoka Oman alipokuwa anachezea klabu ya Fanja SC.
  Awali, kulikuwa kuna taaifa kwamba Lyanga alisajiliwa Singida United Januari mwaka huu wakati akiwa hajamaliza mkataba Fanja FC.
  Mtendaji Mkuu wa Singida United, Sanga Festo amesema kwamba ni kweli Lyanga alikuwa hamaliza mkataba Fanja, lakini walimalizana na kjlabu yake na ikamruhusu kuondoka.
  "Sisi tulifanya jitihada za kuzungumza na Fanja, tukawalipa fedha wakatupa na barua ya kumruhusu kuondoka,"amesema.
  Danny Lyanga (katikati) amekwama kucheza Singida United tangu asajiliwe Januari kutokana na kukosa ITC 

  Sanga amesema kwamba pamoja na kumalizana na Fanja SC, lakini walichelewa kutuma maombi ya ITC hadi dirisha la usajili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara lilipofungwa.
  Amesema kutokana na kuchelewa kutumwa kwa ITC hiyo, sasa mshambuliaji huyo atalazimika kusubiri hadi msimu ujao kucheza Ligi Kuu.
  Ikumbukwe, Lyanga aliyekwenda Fanja akitokea Simba SC ya Tanzania, amecheza michuano ya Kombe la Mapinduzi tu tangu asajiliwe Singida United mwezi Januari. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED WAMALIZANA NA FANJA KUHUSU DANNY LYANGA LAKINI KUCHEZA MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top