• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 27, 2018

  LECHANTRE AWAPA PROGRAMU MAALUM MBONDE, NIYONZIMA SIMBA SC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa Pierre Lechantre amewapa programu maalum ya wiki moja, nyota wake wawili, beki mzawa Salim Mbonde na kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima na kwa ajili ya kujiweka fiti dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Simba ambao watakuwa wenyeji katika mchezo huo utakaopigwa, Aprili 29, mwaka huu, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, huku wachezaji hao wakitarajiwa kuongeza nguvu baada ya kupona majeraha yao.
  Pierre Lechantre amewapa programu maalum ya wiki moja Salim Mbonde na Haruna Niyonzima  

  Pierre aliiambia Bin Zubeiry Sports – Online jana kwamba nyota wake hao wamerejea na kuanza mazoezi mepesi lakini hataweza kuwatumia katika mchezo wao dhidi ya Njombe Mji watakaocheza Aprili 3, Mwaka huu.
  Alisema kutokana na kutowatumia katika mchezo huo, amehakikisha kuwapa Program maalum kwa muda wa wiki moja hadi mbili kuwa fiti na kurejea katika ubora wao na huenda kuwatumia katika mchezo unaofuata.
  “Wanaendelea vizuri leo (Jana) wameanza mazoezi ya viungo na kuzunguka uwanja kwa kuweka mwili fiti, pia watakuwa na program yao na baada ya wiki moja au mbili watakuwa fiti na kuanza kucheza mechi zinazokuja,” alisema Pierre.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LECHANTRE AWAPA PROGRAMU MAALUM MBONDE, NIYONZIMA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top