• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 24, 2018

  NJOMBE MJI WAGOMA KUCHEZA NA SIMBA APRILI 3 WAKO TAYARI KUJITOA LIGI KUU HAWATAKI KUBURUZAWA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Njombe Mji FC umesema haujapokea taarifa yeyote kuhusu mabadiliko ya terehe mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba SC kusogezwa Aprili 3, mwaka huu.
  Msemaji wa Njombe Mji FC, Hassan Mancho, amesema kwamba taarifa zinazosambazwa mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari, mpaka sasa hazina uthibitisho wowote.
  “Kanuni ya Ligi Kuu inatamka kwamba taarifa za mabadiliko ya mchezo zitatolewa kwa klabu siku 14 kabla ya mchezo husika. Timu ya Njombe mji haijapokea taarifa kuhusu mchezo huo kuchezwa Aprili 3, 2018,”amesema.
  Njombe Mji FC hawajapokea taarifa ya mabadiliko ya ratiba ya mchezo wao dhidi ya Simba SC 

  “Hii itakuwa njia ya kutuondoa kwenye ligi, haiwezekani tukacheze Shinyanga, siku mbili halafu turudi Njombe kisha turudi tena Shinyanga siku mbili baadaye. Kanuni inataka tupate taarifa siku kumi na nne kabla, leo hata tukipewa kesho basi siku hizo hazikidhi kwa mujibu wa kanuni" amesema Macho.
  Kwa sasa inajiandaa na safari ya Shinyanga kwa michezo miwili dhidi ya Stand United, wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) Machi 30 na wa Ligi Kuu Aprili 8, zote zikipigwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
  Baada ya hapo, Njombe wanasema ratiba itawapeleka Mwanza kwa mchezo na Mbao Aprili 11, kabla ya kwenda Dar es Salaam kumenyana na Azam FC Aprili 15 kisha kurejea nyumbani mjini Mjombe kucheza na Ndanda FC.
  “Njombe Mji FC inawaomba kupuuza taarifa hizo zisizokuwa rasmi huku ikijikita katika mikakati ya kupata matokeo kwenye mechi za ugenini kama zilivyoorodheshwa hapo juu. Aidha, uongozi huo umesema TFF waiamulie jambo moja la kuitoa kwenye ASFC au Ligi Kuu, tujitoe ASFC au tuondolewe kwenye ligi,”amesema.
  Awali Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliusogeza mbele mchezo kati ya Njombe Mji FC na Simba SC uliopangwa kufanyika Machi 11 Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe.
  Hiyo ilifuatia Simba kuomba mchezo huo uahirishwe ili wapate fursa nzuri ya maandalizi kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry mjini Port Said Machi 17.
  Simba ililazimisha sare ya 0-0 na Al Masry Machi 17 mjini Port Said na kutolewa kwa mabao ya ugenini baada ya sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na sasa inarejesha nguvu zake kwenye Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NJOMBE MJI WAGOMA KUCHEZA NA SIMBA APRILI 3 WAKO TAYARI KUJITOA LIGI KUU HAWATAKI KUBURUZAWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top