• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 20, 2018

  RONALDO ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA KIUME URENO

  NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kiume wa Mwaka 2017 nchini Ureno.
  Katika tamasha lililofanyika usiku wa jana mjini Lisbon, Ronaldo aliwapiku, kiungo wa Manchester City, Bernardo Silva na kipa wa Sporting Lisbon, Rui Patricio kutwaa tuzo hiyo.
  Ronaldo ameshinda tuzo hiyo baada ya kuisaidia Real kushinda mataji yote, La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo mwaka 2017. 

  Cristiano Ronaldo akiwa na mpenzi wake, Georgina Rodriguez tayari kubeba tuzo yake ya Mwanasoka Bora wa Kiume Ureno PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Akiwa ameongozana na mpenzi wake, Georgina Rodriguez, na wakala wake, Jorge Mendes, Ronaldo alipokea tuzo hiyo kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), Aleksander Ceferin.
  Alipata asilimia 65 ya kura zote, dhidi ya asilimia 18 za Patricio na asilimia 17 za Bernardo na baada ya hapo, Ronaldo akasema: "Ni tuzo ya wenzangu wote pia, 2017 ulikuwa mwaka mzuri, usiosahaulika kwa mafanikio ya pamoja na binafsi. Pia naitoa tuzo hiii kwa watoto wangu wanne, ni rekdi nyingine, watoto watatu ndani ya miezi mitatu,"amesema.
  Kocha wa Monaco, Leonardo Jardim alishinda tuzo ya Kocha Bora baada ya kuiongoza timu hiyo ya Ufaransa kushinda taji la Ligue 1 na kufika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameshinda tuzo ya Vasco da Gama kwa kuitangaza soka ya Ureno kimataifa. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA KIUME URENO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top