• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 28, 2018

  NGOMA ANAENDELEA KUIMARIKA KAMBINI YANGA MOROGORO KUELEKEA MECHI NA SINGIDA JUMAPILI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Mzimbabwe wa Yanga SC, Donald Ngoma anaendelea kuimarika katika kambi ya timu hiyo mjini Morogoro kujiandaa na mchezo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation (ASFC) Aprili 1, mwaka huu.
  Yanga watakuwa wageni wa Singida United katika Robo Fainali ya mwisho ya Azam Sports Federation Jumapili Uwanja wa Namfua mjini Singida na katika kujiandaa na mechi hiyo wameweka kambi Morogoro.
  Majeruhi wa muda mrefu, Ngoma ni miongoni mwa wachezaji waliopo kambini Morogoro na Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kwamba Mzimbabwe huyo anaendelea vizuri.
  Donad Ngoma aliumia Septemba 30, mwaka jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam

  Saleh amesema Ngoma ameshiriki mazoezi na wenzake kikamilifu kwa siku zote mbili chini ya kocha Mkuu, Mzambia George Lwandamina.
  Meneja huyo amesema kwamba Ngoma amekuwa akifanya mazoezi yote yanayotolewa na kocha wake ikiwa kupiga mashuti,  mipira ya faulo pamoja na mbinu za kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo.
  "Ngoma anaendelea vizuri, ameungana na wenzake kwa kufanya mazoezi ya pamoja, kufuatia majukumu ya benchi la ufundi," alisema.
  Meneja huyo alisema hali ya kambi ipo vizuri pamoja na kufanya mazoezi mara mbili kwa siku ikiwemo asubuhi na jioni.
  Donad Ngoma aliumia Septemba 30, mwaka jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Kuhusu hali ya mshambuliaji mwingine majeruhi wa muda mrefu, Mrundi, Amissi Tambwe, Saleh amesema kwamba mchezaji huyo anaendelea na mazoezi mepesi ya viungo mjinj Dar es Salaam ataungana na wenzake timu hiyo itakaporejea kutoka Singida.
  Baada ya mechi na Singida, Yanga SC watarudi Dar es Salaam kwa maandalizi ya mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania tiketi ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika Aprili 7, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGOMA ANAENDELEA KUIMARIKA KAMBINI YANGA MOROGORO KUELEKEA MECHI NA SINGIDA JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top