• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 22, 2018

  MBONDE KUANZA MAZOEZI JUMATATU SIMBA BAADA YA KUTOLEWA NYUZI KUFUATIA AJALI YA PIKIPIKI

  Na Mwandishi Weru, DAR ES SALAAM
  BEKI wa Simba, Salim Mbonde anatarajia kujiunga na wenzake Jumatatu ya wiki ijayo baada ya kupona na kutolewa nyuzi juu ya jicho.
   Mbonde alipata ajali ya pikipiki na kuumia juu ya jicho kidogo kabla ya kushonwa nyuzi tatu, hali iliyosababisha aondolewa kwenye kikosi cha Simba SC kilichokwenda Port Said nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Al Masry.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online, Mbonde alisema amepona majeraha aliyoyapata katika ajali hiyo na kuungana na wenzake.
  Salim Mbonde anatarajia kuanza mazoezi Jumatatu ijayo baada ya kutolewa nyuzi juu ya jicho kufuatia ajali ya pikipiki

  Alisema ataungana na kikosi cha Simba kitakachoendelea na mazoezi siku ya Jumamosi kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Njombe Mji.
  "Kwa sasa niko fiti, natarajia kuungana na wenzangu Jumatatu ya wiki ijayo kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Njombe," alisema Mbonde.
  Alisema atahakikisha anajituma kwa kuonyesha uwezo wake ili amshawishi kocha kumpa nafasi ndani ya kikosi cha kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBONDE KUANZA MAZOEZI JUMATATU SIMBA BAADA YA KUTOLEWA NYUZI KUFUATIA AJALI YA PIKIPIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top