• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 27, 2018

  LWANDAMINA AWAPA MAZOEZI YA NGUVU YANGA MOROGORO WAIPIGE SINGIDA NAMFUA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KATIKA kuhakikisha harudii makosa ya awali, Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina ameamua kuwazidishia dozi wachezaji wake, baada ya mara moja na sasa kuwafanyisha mara mbili kwa siku.
  Yanga walionda jijini na kuelekea kujichimbia Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao dhidi ya Singida United, kujiandaa na Robo Fainali Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Kikosi cha timu hiyo kiliendelea na mazoezi yake jana asubuhi Uwanja wa Jamhuri, mkoani humo na jioni kuendelea na programu hiyo.
  Kocha Mzambia wa Yanga SC, George Lwandamina hataki kurudia makosa  

  Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema kikosi chao kinaendelea vyema na mazoezi ikiwemo mshambuliaji wao, Donald Ngoma aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu kujumuika na timu hiyo.
  Alisema wachezaji wote wako vizuri na morali ya ushindi, hivyo kuongeza muda wa mazoezi kutachangia kwa kufanya vyema katika mchezo huo.
  “Kikosi kipo vizuri, tayari Lwandamina ameongeza muda wa mazoezi badala ya mara mmoja sasa tutafanya mara mbili kwa siku asubuhi na jioni,” alisema Hafidh.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LWANDAMINA AWAPA MAZOEZI YA NGUVU YANGA MOROGORO WAIPIGE SINGIDA NAMFUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top