• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 29, 2018

  KIINGILIO NGORONGORO HEROES NA KONGO SH 1,000 TU, TUJITOKEZE KWA WINGI JUMAMOSI TUKAWASAPOTI VIJANA KUFUZU AFCON U-20

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIINGILIO cha katika mchezo wa kwanza wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON U20) 2019 nchini Niger kati ya wenyeji Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jumamosi kitakuwa Sh. 1,000.
  Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo katika mazungumzo na Bin Zubeiry Sports – Online leo mjini Dar es Salaam.
  Ndimbo amesema kwamba kiingilio hicho kitahusu majukwaa ya mzunguko tu, wakati majukwaa ya VIP A, B na C watu wataingia kwa Sh. 3,000. 
  Kikosi cha DRC kimewasili jana usiku mjini Dar es Salaam na kesho jioni kitafanya mazoezi Uwanja wa Taifa kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.
  Kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Ammy Ninje atawania ushindi wa tatu mfululizo Jumamosi 

  Ngorongoro Heroes iliyo chini ya kocha Ammy Conrad Ninje itaingia kwenye mchezo wa Jumamosi ikitoka kushinda mechi mbili za kujipima dhidi ya Morocco 1-0 na Msumbiji 2-1.
  Na kwa ujumla vijana wasiozidi umri wa miaka wa 20 wa DRC na Tanzania watakutana keshokutwa ikiwa ni siku tat utu baada ya kaka zao kukutana na Taifa Stars kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Chui wa Kinshasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIINGILIO NGORONGORO HEROES NA KONGO SH 1,000 TU, TUJITOKEZE KWA WINGI JUMAMOSI TUKAWASAPOTI VIJANA KUFUZU AFCON U-20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top