• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 30, 2018

  FEISAL YU TAYARI KUTUA POPOTE YANGA AU SINGIDA UNITED, ANAANGALIA MASLAHI

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KIUNGO chipukizi Mzanzibari, Feisal Salum `Fei Toto` wa JKU ya nyumbani, Unguja amesema kwamba popote anaweza kutua kati ya Singida United na Yanga, itategemea na maslahi.
  Fei alionekana na kiongozi mmoja wa Singida United Jumanne Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam baada ya mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya wenyeji, Tanzania ‘Taifa Stars’ na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Fei Toto alikuwa benchi kwa dakika zote 90 siku hiyo Taifa Stars ikiibuka na ushindi wa 2-0, mabao ya Nahodha na mshambuliaji Mbwana Samatta na winga Shiza Kichuya, yote kipindi cha pili – na baada ya mechi akaenda kuzungumza na bosi wa Singida, jambo ambalo lilitafsiriwa ni mipango ya usajili. 
  Feisal Salum `Fei Toto` anaweza kutua popote kati ya Singida United na Yanga, itategemea na maslahi.

  Lakini Singida United wanajitokeza kama timu nyingine inayowania saini ya Feisal huku kukiwa tayari kuna uzumi kwamba kiungo huyo yuko mbioni kujiunga na mabingwa wa Tanzania, Yanga SC waliovutiwa naye tangu mapema Januari kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar. 
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Fei Toto alikiri kuzungumza na viongozi wa timu zote mbili, kwa wakati tofauti na kusema kwamba Singida United ndiyo wameonyesha dhamira ya dhati zaidi ya kuhitaji huduma zake.
  Alisema kwa upande wake yupo tayari kujiunga na timu yoyote kati ya hizo, kwani mkataba wake na JKU haumfungi kulingana na kueleza kwamba watamuachia endapo kuna timu itamuhitaji.
  “Nimeongoea na Yanga kabla sijarejea nyumbani Zanzibar, pia leo (Jana) viongozi wa Singida wamenipigia simu kunisisitizia juu ya dhamira yao, kwa upande wangu yeyote atakayekuja vizuri nitasaini,
  “Kwa sasa sitaweka hadharani dau, kwani ninachoangalia ni maslahi, kama Yanga au Singida mmoja wapo atakuja na kile kitakachoniridhisha nitasaini moja ya timu hizo,” amesema Fei Toto.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FEISAL YU TAYARI KUTUA POPOTE YANGA AU SINGIDA UNITED, ANAANGALIA MASLAHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top