• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 27, 2018

  MRUNDI WA STAND UNITED ASEMA NJOMBE MJ FC KIFO CHAO KIMEWADIA ASFC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAADA ya kuiondoa Dodoma FC katika hatua ya 16 bora, Kocha Mkuu wa Stand United, Mrundi Niyongabo Almasi ametamba kuhakikisha vijana wake kufanya vyema katika mchezo wao dhidi ya Njombe Mji Robo Fainali ya Azam Sporta Federation (ASFC)
  Stand itaikaribisha Njombe Mji FC Machi 30, mwaka huu  Uwanja CCM Kambarage, mjini Shinyanga na Almasi alisema kikosi chake kimeandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha wanatumia vema uwanja wa nyumbani kupata ushindi katika mchezo huo.
  Alisema kuwa timu hiyo imejipanga kuhakikisha inafanya maajabu ya kuchukua ubingwa na kuiwakilisha nchi katika michuano Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
   “Mikakati yetu ni kuhakikisha tunafanya vyema katika mchezo huu, ili kuingia katika hatua ya nusu fainali, kwa lengo la kusonga mbele hadi kucheza fainali, ili kupata nafasi ya kuwakilisha vyema nchini kimataifa mwakani,” alisema Almasi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MRUNDI WA STAND UNITED ASEMA NJOMBE MJ FC KIFO CHAO KIMEWADIA ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top