• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 25, 2018

  DRC WAWASILI NA KIKOSI CHA NYOTA KIBAO WA ULAYA KUIVAA STARS JUMANNE, BUKAMBU, BELAISE NDANI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), maarufu kama The Leopards (Chui) kwa jina la utani kimewasili mjini Dar es Salaam asubuhi ya leo tayari kwa mchezo wa kirafki dhidi ya wenyeji, Tanzania, Taifa Stars Jumanne Uwanja wa Taifa, Jijini.
  DRC iliyo chini ya kocha, mzalendo Jean-Florent Ikwange Ibenge imewasili na nyota wake wote akiwemo mwansoka ghali zaidi Afrika kwa sasa, Cedric Bakambu aliyejiunga na Beijing Guoan ya China kwa dau la Pauni Milioni 65 kutoka Villarreal ya Hispania, Bolasie Yannick, Chancel Mbemba na Masuaku Arther wanaocheza Ligi Kuu ya England.
  Taifa Stars ya kocha mzalendo pia, Salum Mayanga itacheza mechi ya pili mfululizo ya kujipima nguvu ndani ya siku sita baada ya Alhamisi kufungwa 4-1 na Algeria mjini Algiers.
  Wachezaji wa DRC wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mapema leo mjini Dar es Salaam
  Hiyo ni sehemu ya maandalizi mechi zake za Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon, ambako imepangwa na pamoja na Lethoto, Uganda na Cape Verde.
  Kikosi kamili cha DRC kilichowasili leo ni makipa; Parfait Mandanda (Charleroi, Ufaransa), Joel Kiassumbua (Lugano, Italia) na Matampi Ley.
  Mabeki; Issama Mpeko (TP Mazembe), Ikoko Jordan (EAG, Ufaransa), Nsakala Fabrice (Alayanspor, Uturuki), Ngonda Glody (AS Vita), Masuaka Arthur (West Ham, England), Chancel Mbemba (Newcastle United, England), Moke Will (Konyaspor, Uturuki), Bangala Yannick ( AS Vita), Luyindama Christian (Standard, Ubelgiji), Mulumbu Youssouf (Kilmanock, Scotland) na Lema Mabidi (Raja Casablanca, Morrocco).
  Viungo; Kebano Neeskens (Fulham, England), Giannelli Imbula (Toulouse, Ufaransa), Maghoma Jacques (Birmingham, England ) na Kakuta Gael (Amiens, Ufaransa).
  Washambuliaji; Balasie Yannick (Everton, England), Kabananga Junior (Al Nassr, Saudi Arabia), Mubele Fiemin (Toulouse, Ufaransa ), Paul Jose Mpaku (Standard Liege, Ubelgiji), Cedric Bakambu (Beijing, China), Afobe Benik (Wolves, England ) Assombalonga Britt (Middlesbrough, England) na Thibola Aaron (Kilmanock, Scotland ).
  Mchezo utaanza Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kwa kiingilio cha Sh. 1,000 majukwaa ya mzunguko na Sh. 5,000 kwa VIP.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DRC WAWASILI NA KIKOSI CHA NYOTA KIBAO WA ULAYA KUIVAA STARS JUMANNE, BUKAMBU, BELAISE NDANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top