• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 19, 2018

  KOCHA MAJI MAJI AWANYIMA MAPUMZIKO WACHEZAJI WAJIFUE KUINUSURU TIMU KUSHUKA DARAJA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KITENDO cha Maji Maji kushika nafasi ya pili kutoka mkiani, imesababisha wachezaji wa timu hiyo kutopata mapumziko mafupi kama ilivyo zingine zinashiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Kocha Mkuu wa timu hiyo, Habib Kondo alisema katika kipindi hiki cha mapumziko ya ligi hiyo kupisha ratiba ya timu ya taifa na michuano ya kombe la shirikisho Tanzania, wamekuwa wakiendelea na mazoezi.
  Alisema kulingana na nafasi walikuwepo katika msimamo wa ligi hiyo,  ameamua kufanya hivyo ili kuendelea mazoezi kwa ajili ya kujiweka fiti na kuongeza wachezaji vijana kutoka kikosi B kutia nguvu ndani ya timu hiyo.
  “Machi 8, tunatarajia kucheza na Mbao FC, katika mechi hiyo kikosi chetu kitaanza kuonekana kipya kwa sababu kuna wachezaji wengi wa timu ‘B’ tumewajumuisha ili kuziba mapengo ya wachezaji walioondoka,” alisema Kondo.
  Alisema ana imani mazoezi hayo yatawajenga kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo iliyobakia kwa ajili ya kujiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea kubaki katika ligi hiyo.
  Kwa sasa Maji Maji inashika mkia katika Ligi ya timu 16, ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi 22.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA MAJI MAJI AWANYIMA MAPUMZIKO WACHEZAJI WAJIFUE KUINUSURU TIMU KUSHUKA DARAJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top