• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 31, 2018

  JKT TANZANIA YAIZIMA PRISONS PALE PALE SOKOINE NA KWENDA NUSU FAINALI ASFC

  TIMU ya JKT Tanzania imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya leo.
  JKT iliyorejea Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuelekea msimu ujao, iliizima kabisa Prisons leo Sokoine na kupata ushindi huo mzuri kwa mabao ya Ally Ahmed dakika ya 43 na Hassan Matelema dakika ya 78.
  JKT ya kocha Bakari Shime inaungana na Stand United iliyotangulia Nusu Fainali jana kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Njombe Mji FC Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga, bao pekee la Abdul Swamad dakika ya 12.
  Hassan Matelema (kushoto) amefunga bao la pili leo dakika ya 78

  JKT sasa itasubiri mshindi wa mchezo wa Robo Fainali ya mwisho kesho, kati ya Singida United na Yanga ikutane naye Nusu Fainali, wakati Stand United iliyomaliza pungufu jana baada ya Nahodha wake, Erick Mulilo kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 80 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano itakutana na mshindi wa mchezo wa leo usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kati ya Azam FC na Mtibwa Sugar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JKT TANZANIA YAIZIMA PRISONS PALE PALE SOKOINE NA KWENDA NUSU FAINALI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top