• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 20, 2018

  MBEYA CITY YAPANIA KULIPA KISASI KWA AZAM MECHI YA MARUDIANO LIGI KUU SOKOINE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAADA ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam FC, Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhani Nsanzurwimo amesema atahakikisha analipa kisasi kwa wapinzani wake hao katika mchezo wao Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Mbeya City itawakaribisha Azam katika mechi ya mzunguko wa pili unaotarajiwa kuchezwa Aprili 8 mwaka huu katika Uwanja wa Sokoine, Mkoani Mbeya.
  Nsanzurwimo ameliambia  kwamba anaendelea na mazoezi kwa ajili ya kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo na kutokubali kupoteza pointi kwa Azam.
  Alisema anahitaji kulipa kisasi kutokana na wapinzani wake hao kupata pointi tatu muhimu katika uwanja wake wa Nyumbani, Azam Complex,  hivyo anahitaji kulipa kisasi kwao.
  “Siwadharau Azam ni timu nzuri, pia nahitaji kutumia vyema uwanja wetu wa nyumbani, wenzetu wanahitaji kupata ushindi kwenda juu, kwetu tunahitaji pointi hizo kujinasua katika nafasi tuliopo sasa,” alisema.
  Nsanzurwimo alisema hadi sasa anamajeruhi mmoja ambaye ni Erick Kiyaruzi anayetibiwa chini ya mtalaam wa viungo, Daktari Gilbert Kigadye.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAPANIA KULIPA KISASI KWA AZAM MECHI YA MARUDIANO LIGI KUU SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top