• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 28, 2018

  KICHUYA ASEMA SHUGHULI YAKE YA JANA NI SALAMU KWA NJOMBE MJI FC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba, Shiza Kichuya amesema kwamba ana hamu Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara irejee mapema ili afanye vitu.
  Kichuya alisema hayo katika mahojiano maalum na Bin Zubeiry Sports - Online jana muda mfupi tu baada ya kuisaidia Tanzania kushinda 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa kirafiki.
  Jana Kichuya alimsetia Nahodha Mbwana Samatta kuifungia Taifa Stars bao la kwanza dakika ya 74, kabla ya yeye mwenyewe kufunga la pili dakika ya 88 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Akiwa mwenye furaha, baada ya mchezo huo, Kichuya alisema; "Sasa nimewasha moto, Ligi Kuu irudi sasa niendeleze moto wangu,".
  Shiza Kichuya baada ya kuifungia Taifa Stars bao la pili jana Uwanja wa Taifa
    
  Baada ya mchezo huo kumalizika Kichuya alisema kasi aliyoonyesha katika mchezo huo anahamishia ndani ya kikosi cha klabu yake, utakayocheza na Njombe Mji, April 3 mwaka huu.
  Alisema kwa siku zilizosalia anaona ligi hiyo inachelewa kulingana na morali aliyokuwa nayo.
  "VPL unachelewa miguu unawasha," alisema Kichuya.
  Kauli huyo ya Kichuya ni salamu anazo kwa wapinzani wao kwamba yupo vizuri kusaidia timu yake kupata pointi muhimu ili kutwaa taji la Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KICHUYA ASEMA SHUGHULI YAKE YA JANA NI SALAMU KWA NJOMBE MJI FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top