// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); EVRA ASIMAMISHWA MARSEILLE KWA KUMPIGA TEKE SHABIKI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE EVRA ASIMAMISHWA MARSEILLE KWA KUMPIGA TEKE SHABIKI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, November 04, 2017

    EVRA ASIMAMISHWA MARSEILLE KWA KUMPIGA TEKE SHABIKI

    KLABU ya Marseille imemsimamisha Patrice Evra baada ya beki huyo wa kushoto kumpiga teke shabiki wa timu hiyo kabla ya mchezo wa Kundi I Europa League dhidi ya wenyehi Vitoria Guimaraes usiku wa Alhamisi.
    Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United mwenye umri wa miaka 36 alikasirika na kumpiga teke shabiki akidai alimtolea maneno ya kashfa.
    Timu hiyo ya Ligue 1 imesema kwamba ilimhoji Evra kabla ya kuchukua uamuzi huo.
    Taarifa ilisema kwamba; "Jacques-Henri Eyraud, rais wa Olympique de Marseille, alikutana na Patrice Evra na kumuarifu juu ya uzito wa kosa lake na hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi yake.

    Klabu ya Marseille imemsimamisha Patrice Evra baada ya kumpiga shabiki   PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: EVRA ASIMAMISHWA MARSEILLE KWA KUMPIGA TEKE SHABIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top