• HABARI MPYA

  Tuesday, October 10, 2017

  NDUDA ARUHUSIWA KUONDOKA HOSPITALI INDIA BAADA YA MATIBABU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIPA namba mbili wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Said Mohammed ‘Nduda’ juzi aliruhusiwa kuondoka katika hospitali aliyotibiwa goti nchini India, siku nne tu baada ya kuwasili.
  Nduda ambaye amekuwa akitumia akaunti yake ya Instagram kuonyesha namna anavyofurahia maisha katika klabu yake mpya, licha ya kuwa majeruhi kwa sasa aliposti picha akiwa na wafanyakazi wa hospitali aliyokuwa anatibiwa pamoja na maelezo; “Asante Mungu baada ya kurusiwa hospitali nipo na wanangu akina Sharukh Khan, nimeishi nao safi, kidogo tu wamenimiss, asante Mungu,”.
  Hata hivyo, alipoulizwa na Bin Zubeiry Sports – Online leo juu ya maendeleo ya kipa huyo baada ya upasuaji, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Hajji Manara alisema anachofahamu Nduda bado yupo India anaendelea na matibabu.
  Said Mohammed ameposti video akiwa anaechezea dola za Kimarekani kwa furaha na rafiki zake


  Hii nu picha Said Mohammed aliposti akisema amehusiwa kuondoka hospitali

  Said Mohammed akionyesha Timberland lake na saa kali kwenye gari aina ya IST 

  Nduda amekuwa akiposti video na picha tofauti kuonyesha furaha yake akiwa na Wekundu wa Msimbazi, baada ya awali kuchezea Maji Maji ya Songea, Yanga ya Dar es Salaam na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
  Jana Nduda aliposti video akiwa na mavazi aliyovaa India siku anasema ameruhusiwa kutoka hospitali, lakini akiwa kwenye gari na rafiki zake wawili wamefungulia ‘muziki mkubwa’ huku akionyesha noti nyingi za dola za Kimarekani.
  Rafiki yake mmoja naye akatoa burungutu la fedha za Kitanzania kuonyesha – kuashiria kwamba wapo katika wakati mzuri sana wa furaha. 
  Septemba 28, mwaka huu Ndunda aliposti picha yake akiwa ndani ya gari inayoonekana ni ya kwake, aina ya IST akionyesha alivyopendeza kimavazi na kiatu chake kizuri cha Timberland na saa sambamba na maelezo; “Wozaa,”.
  Siku moja kabla, Nduda aliposti picha akiwa kwenye gari hiyo hiyo ya IST nyeupe ameweka kikombe kidogo cha kahawa mlangoni inayoonekana alikuwa anakunywa. 
  Ikumbukwe Nduda aliyesajiliwa Simba Julai mwaka huu akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, hajacheza mechi yoyote ya Ligi Kuu msimu huu kutokana na maumivu ya goti aliyoyapata Agosti mazoezini.
  Simba ilivutiwa na Nduda na kumsajili baada ya kudaka vizuri katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa Kombe la COSAFA dhidi ya Lesotho Julai 7, mwaka huu mjini Rusternburg, Afrika Kusini Taifa Stars ikishinda kwa penalti baada ya sare ya 0-0. 
  Na Nduda akashinda tuzo ya kipa bora wa mashindano hayo baada ya kazi yake nzuri kwenye mchezo huo mmoja tu, kiasi cha kuwashawishi na Simba kumsajili na kumuunganisha na kipa namba wa Taifa Stars, Aishi Manula.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDUDA ARUHUSIWA KUONDOKA HOSPITALI INDIA BAADA YA MATIBABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top