• HABARI MPYA

  Tuesday, October 10, 2017

  YANGA YATHIBITISHA NGOMA ATAKOSEKANA DHIDI YA KAGERA SUGAR BUKOBA JUMAMOSI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Yanga imethibitisha mshambuliaji wake Mzimbabwe, Donald Dombo Ngoma hataweza kusafiri na timu kwenda Bukoba kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar Jumamosi.
  Ngoma aliumia misuli midogo ya paja katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu wa Yanga ikilazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar Oktoba 1 na baada ya kufanyiwa vipimo na kutibiwa Oktoba 3, alitarajiwa kuanza mazoezi mepesi leo.
  Lakini akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Msemaji wa Yanga, Dissmas Ten amesema kwamba Ngoma anahitaji muda zaidi wa mapumzikonna hatasafiri kwenda Bukoba.
  “Unajua wakati mwingine vipimo vinafanyika na muda unatolewa wa mapumziko, lakini ni makadirio tu ambayo yanaweza kuongezeka, hivyo na yeye anahitaji muda zaidi,” amesemna Tena.
  Yanga imethibitisha Donald Ngoma hataweza kusafiri na timu kwenda Bukoba kwa ajili ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar Jumamosi

  Siku hiyo, Ngoma aliondoka uwanjani anachechemea dakika ya 77 Yanga ikilazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Mahadhi.
  Na baada ya hapo, mchezaji huyo akaenda kufanyiwa vipimo Oktoba 3 na kugundulika misuli ya ndani ya paja ilivutika siku hiyo na kumsababishia maumivu kwa mujibu wa Daktari wa Yanga, Edward Bavu.
  Daktari huyo wa Yanga amesema kwamba hayo ni maumivu mapya kabisa kwa Ngoma tofauti na yale yaliyomuweka nje kwa muda mrefu msimu uliopita ya goti.
  Baada ya kusimama kwa siku 10 kupisha mechi za kimataifa za kufuzu Kombe la Dunia na za kirafiki kwa nchi ambazo zimekwishatolewa kwenye mbio za Urusi 2018, ikiwemo Tanzania, Ligi Kuu inatarajiwa kurejea wikiendi hii na Yanga watakuwa wageni wa Kagera Sugar, wakati mahasimu wao, Simba Jumapili watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru, Dar es Dalaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YATHIBITISHA NGOMA ATAKOSEKANA DHIDI YA KAGERA SUGAR BUKOBA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top