• HABARI MPYA

  Saturday, October 07, 2017

  JULIANA SHONZA NAIBU WAZIRI MPYA WA MICHEZO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  JULIANA Daniel Shonza atakuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, akichukua nafasi ya Mama Anastazia Wambura kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magiguku leo. Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu mjini Dar es Salaam leo, imesema kwamba Mama Juliana Shonza mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) pamoja wateule wengine wapya wa Baraza la Waziri wataapishwa Jumatatu.
  Juliana Daniel Shonza ndiye Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo

  Juliana Shonza atakuwa chini ya Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ambaye aliingia ofisini Machi 23, mwaka huu akichukua nafasi ya Nape Moses Nnauye aliyeondolewa.
  Nape na Mama Anastazia Wambura walikuwa wateule wa kwanza wa Rais Dk Magufuli katika Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo baada ya kuingia Ikulu Novemba mwaka juzi kwa tiketi ya CCM, akimuangusha aliyekuwa mpinzani wake mkuu, Edward Ngoyai Lowassa wa UKAWA.
  Kisiasa, Juliana Shonza aliibukia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambako alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA) kuanzia mwaka 2011, baada ya kuwa mwasisi wa Jumuiya ya wanafunzi wafuasi wa CHADEMA (CHASO) kuanzia mwaka 2010.
  Aliasisi CHASO akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambako alihitimu Shahada ya Sosholojia mwaka 2011, kabla ya Chuo Kikuu cha Dodoma kufanya Shahada ya Uzamivu alikohitimu mwaka 2015.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JULIANA SHONZA NAIBU WAZIRI MPYA WA MICHEZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top