• HABARI MPYA

  Saturday, October 07, 2017

  SAMATTA: TUNAPASWA KUSHINDA LEO TURUDI JUU FIFA

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta amesema ni muhimu kwao kushinda mchezo wa leo dhidi ya Malawi ili kujirudisha juu kwenye viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
  Taifa Stars watateremka kwenye Uwanja wa Uhuru kwa mara ya pili mfululizo leo kumenyana na The Flames kuanzia Saa 10:00 jioni katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa ambao utaonyeshwa moja kwa moja na chaneli ya Azam Sports 2 ya Azam TV.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari jana mjini Dar es Salaam, Samatta alisema kwamba ni muhimu kwa Taifa Stars kushinda ili kujirudisha juu kwa kwenye viwango vya FIFA baada kuteremka kutokana na matokeo mabaya.  
  Nahodha Mbwana Samatta (kushoto) amesema ni muhimu Taifa Stars kushinda leo dhidi ya Malawi ili kujirudisha juu kwenye viwango vya FIFA

  Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Shaaban Mayanga amesema kwamba mchezo utakuwa mgumu kwa sababu Malawi ni timu nzuri na walikutana nayo mwezi Juni kwenye michuano ya Kombe la COSAFA nchini Afrika Kusini. 
  Naye kocha wa Malawi, Mholanzi Ronny Van Geneugden amesema mchezo huo ni fursa nzuri kwa wachezaji wapya aliowaita kuonyesha uwezo. 
  Nahodha wa Malawi, Robert Ng’ambi anayechezea Platinums Stars ya Afrika Kusini amesema anatarajia mchezo mzuri na mgumu kesho, kwa sababu wachezaji wa timu hizo wanafahamiana.
  Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana Jumapili ya Juni 25 mjini Rysternburg, Afrika Kusini kwenye Kombe la COSAFA, Tanzania iliichapa Malawi 2-0, mabao yote yakifungwa na Shiza Ramadhani Kichuya dakkika za 13 na 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA: TUNAPASWA KUSHINDA LEO TURUDI JUU FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top